Wana Mtandi Nyumbani kwa Akwilapo

Wana Mtandi nyumbani kwa Dkt Akwilapo wamezima zote na wamewasha kijani.

Kwenye mkutano uliofanyika tarehe 16/09/2025 Wajumbe na wanachama wa CCM kata ya Mtandi Wamefunga mkataba wa kutafuta kura kwa chama cha mapinduzi ndani na nje ya chama.

Dkt Akwilapo amewahakikishia wana Mtandi kuwa ana dhamira kubwa ya kuibadilisha Masasi ili ifanane na ukubwa na umaarufu wa jina lake kwa kuhakikisha yale yote yaliyo ainishwa kwenye ilani yanatekelezwa na kufanyiwa kazi. Atahakikisha anashughulikia kwa ukaribu masuala ya elimu, afya, miundo mbinu, kilimo na kuunganisha wana masasi ili wawe kitu kimoja kwa sababu imani yake bila umoja hakuna maendeleo

1 thought on “Wana Mtandi Nyumbani kwa Akwilapo”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top